
NA EUNICE KANUMBA –SHINYANGA
MKUU wa wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro ametoa maagizo kwa mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Shinyanga Dr. Kalekwa Kasanga kushughulikia Hoja 50 zilizoibuliwa katika ripoti iliyopita ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) ambazo bado utekelezaji wake unaendelea na kwamba vipatikane vielelezo vyenye majawabu ya hoja hizo hadi ifikapo tarehe 18 june 2025 ili hoja hizo ziweze kufungwa kwa mujibu wa taratibu.

Wakili Mtatiro amebainisha hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha leo Juni 11, 2025 wakati akihutubia baraza maalum la madiwani lililoketi kupitia taarifa ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) zilizokaguliwa katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2024.
Awali akisoma hoja hizo zilizoibuliwa na katika ripoti ya CAG mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Shinyanga Dr. Kalekwa Kasanga amesema halmashauri hiyo ilipata hati safi katika hesabu za mwaka wa fedha 2023/2024 huku akianisha kuwa katika mwaka huo ziliibuliwa hoja 52 ambapo hoja mbili zimefungwa na kubaki hoja 50 ambazo bado utekelezaji wake unaendelea.

Aidha, Dr. Kasanga pia amehaidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa Dc Mtatiro na kwamba wanakwenda kutekeleza maagizo hayo ili ifikapo tarehe 18 june ili hoja zenye uwezekano wa kufungwa ziweze kufanyiwa mchakato wa kufungwa na kumalizika kabisa
“Mheshimiwa Mwenyekiti napenda kukutaarifu kwamba, kwa hesabu za mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2024, Halmashauri yako imepata Hati Safi,” amesema Dk.Kasanga.
Akizungumza pia katika kikao hicho, Afisa kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Mkoa wa Shinyanga CPA Yusuph Mabwe, amesema kwamba utekelezaji wa mapendekezo ya hoja hizo kasi yake iongezeke sababu yanatekelezeka.
Katika hatua nyingine Halamashuri hiyo ya wilaya ya Shinyanga sambamba na kupata Hati Safi, lakini pia imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa kukusanya asilimia 106 ya mapato kwa mwaka wa fedha uliopita.