DC MTATIRO AENDELEZA KILINIKI USIKILIZAJI KERO, MIGOGORO YA WANANCHI

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, wakili Julius Mtatiro ameendelea na utaratibu wake wa Kiliniki ya kusikiliza kero na migogoro ya wananchi  kwa mafanikio makubwa,  ambapo wananchi Zaidi ya mia mbili wamejitokeza kuwasilisha  changamoto zao, huku migogoro ya ardhi ikiongoza miongoni mwa kero zilizowasilishwa.


Kliniki hiyo, imefanyika katika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ikilenga  kuwapatia wananchi fursa ya kueleza changamoto zao moja kwa moja kwa uongozi wa serikali, na kutafuta suluhu za haraka na za kudumu. 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, wakili Julius Mtatiro.

Akizungumza katika kliniki hiyo, DC Mtatiro ameeleza  umuhimu wa wananchi kupata elimu ya ardhi ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima,ambapo amesema serikali itaendelea kushirikiana na wataalamu wa ardhi pamoja na viongozi wa maeneo husika kuhakikisha wananchi wanapatiwa taarifa sahihi na msaada wa kitaalamu.

Akianisha namna ya kushugulikia changamoto zilizowasilishwa DC Mtatiro amesema wameunda timu tano ambapo kila timu itashugulika na migogoro husika ilipoyangiwa ikiwemo timu ya rufaa itakayohusisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo itakayoshughulikia migogoro yote yenye masilahi mapana kwa wananchi.

Sehemu ya Wananchi waliohudhuria Kliniki hiyo.

Kutokana na kuongoza kwa kero ya migogoro ya aridhi katika kiliniki hiyo DC Mtatiro amesema serikali itasimamia suala la upimaji shirikishi na kwamba migogoro mingi ya aridhi inatokea katika jamii kutokana na ubabe wa baadhi ya watu unaofanywa katika maeneo husika.

“Fulani anamuona mama mmoja ambaye ni mzee na yeye  anataka kujenga ukuta anaingilia eneo lake kwa kuona huyo mama atamfanya nini?na mama anakwenda kushitaki katika ngazi za msingi hatua hazichuliwi na ndio maana tumeanzisha kiliniki hii,” amesema DC Mtatiro.

Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Leila Chipanyanga.

Naye Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Leila Chipanyanga amesema jumla ya migogro waliyopokea ni 78 na kwamba wanaendela na mchakato wa utatuzi wake, ambapo katika migogoro waliyopokea wananchi wengi hawakuiripoti ofisi ya ardhi na badala yake walikimbilia Mahakamani.

Chipanyanga amesema, kisheria mgogoro wowote unapofikishwa Mahakamani haupaswi  kuingiliwa na Ofisi ya ardhi mpaka itakapowasilishwa nakala ya hukumu ya kesi husika, hivyo wameendela kutoa elimu kwa wananchi juu ya sheria za aridhi kwani migogoro mingi pia imetokana na wananchi kutokujua sheria.

“Tunawashuri wananchi kabla hujanunua aridhi  ni muhimu kufika ofisi ya mkurugezi kitengo cha aridhi ili  kujiridhisha kwani kuna watu wananunua maeneo ya masoko, au barabara pindi ukimjulisha kuwa eneo alilonunua si sahihi anahesabu  kama mgogoro lakini huo sio mgogoro,” amesema Chipanyanga.

Nao baadhi  Wananchi waliopata nafasi ya kusikilizwa kero zao na kutatuliwa katika kiliniki hiyo, akiwemo Ally Salum na Foibe Bida  woye wakiwa ni wakazi Manispaa ya Shinyanga, wameishukuru serikali kwa kuanzisha kliniki hiyo, wakisema imewapa matumaini mapya ya kupatiwa haki na suluhu za changamoto zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *