Na Frank Aman – Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba amezindua rasmi Kampeni ya usafi katika Manispaa ya Geita na kuwaasa wananchi wote kujenga desturi ya kufanya usafi kila siku katika makazi yao na maeneo yao ya kazi, biashara na maeneo yanayotumiwa katika shughuli zingine.
Akizungumza wakati wa Zoezi la Usafi katika Manispaa hiyo, DC Komba ameongeza kuwa watu wengi wamejenga mazoea ya kusubiri usafi wa mwisho wa mwezi pekee jambo ambalo linapelekea maeneo mengi ya Manispaa kuwa machafu.

“Desturi hii haikubaliki hata kidogo hivyo wananchi wote wanatakiwa kubadilika kuanzia Sasa titaendrsha Zoezi la Usafi wa Maeneo yetu Kila Siku ya Jumamosi, ikiwa na Lengo la kuweka Manispaa yetu katika Hali ya Usafi,” amesema.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Geita ameeleza kuwa kutakuwa na utaratibu wa kutoa tuzo na pongezi kwa wananchi watakaofanya usafi kwa viwango vinavyokubalika na kutoa onyo na adhabu kwa watakaokaidi zoezi la usafi endelevu.
