DC Kishapu ataoa neno kwa wanaolea watoto

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amesema katika kusimamia ulinzi na maadili ya nchi kwa ustawi na makuzi ya mtoto wamiliki wa shule na vituo vya kulelea watoto wanapaswa kuhakikisha wanatambua viashiria vya vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa watoto wanapokuwa katika maeneo hayo.

Mkude ameyasema hayo leo 20 Septemba 2023 katika uzinduzi wa programu jumuishi ya taifa ya malezi, makazi na maendeleo ya awali ya mtoto mwaka 2021/2022 hadi 2025/26 akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme na kuwataka wamiliki wote wa vituo vya kulelea watoto kuhakikisha wanajisajili kwa kufuata taratibu zinazotakiwa mpaka kufikia Novemba 30 mwaka huu.

Mkude ameongeza kuwa ili kuhakikisha mkoa wa Shinyanga unafanya vizuri na kuwa bora katika utekelezaji wa programu jumuishi amewataka waratibu kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuandaa mpango kazi unaogusa maeneo yote husika ili kuwapa fursa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto watumishi wote na waajiri wa sekta za umma na binfsi.

Naye afisa maendeleo mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale amesema kuwa mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika hii leo mafunzo yataendelea kutolewa kwa wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali ambapo watajifunza kwa undani zaidi juu ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto utakaojumuisha elimu ya shule salama katika kupinga ukatili wa kingono, kisaikolojia na aina zote za ukatili kwa watoto.

a

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *