DC KALLI AWATAKA MADEREVA BODABODA KUEPUKA AJALI ZA KIZEMBE

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Salum Kalli amewataka madereva bodaboda wilayani humo kuhakikisha wanafuata na kuzingatia sheria za usalama barabarani, ili kujiepusha na ajali zinazoweza kutokea kwa uzembe.

Mkuu huyo wa Wilaya alitoa wito huo wakati akizungumza na madereva hao kufuatia elimu iliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya humo kwa ajili ya kuwajengea uwezo juu ya sheria mbalimbali za usalama barabarani.

Mhe. Kalli alisema endapo madereva bodaboda watatii na kuheshimu sheria za usalama barabarani itasaidia sana kupunguza ajali ambazo sio za lazima ambazo zinaepukika hivyo akawataka kuhakikisha wanafuata sheria hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Wilayani humo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Amilton Matagi, alitawataka madereva hao kufuata utaratibu utakaopangwa na Jeshi la Polisi wa kupata mafunzo ya udereva ili kuweza kupata leseni za udereva na bima ambazo zitawasadia kupata haki zao pindi watakapopata changamoto wakati wakitekeleza majukumu yao.

Naye Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Wilayani humo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP) Goodluck Banele aliwataka madereva hao kwenda kuwa mabalozi wazuri kwa kuwaelimisha wengine juu mambo mbalimbali waliyofundishwa hasa uzingatiwaji wa Sheria za usalama barabarani

Nao baadhi ya Madereva waliopata elimu hiyo wameeleza kufurahishwa na elimu iliyotolewa na kuomba iwe inatolewa mara kwa mara ili wote wapate uelewa wa pamoja juu ya sheria hizo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *