Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda amekabidhi Pikipiki 10 kwa vikundi viwili vya Vijana 10 kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na Kikundi cha Umoja Dareda Kati, kukopeshwa milioni 14, huku umoja Kiru Diki ukipata milion 15.
Katika makabidhiano hayo,, Kaganda amesema Serikali kupitia Ilani ya CCM inaendelea kuwawezesha Vijana mikopo isiyo na riba, tofauti na ile ya kibiashara ambayo imekuwa ikiwatesa.

Amesema, “Serikali ina mapenzi ya dhati kwa Vijana wake, ndiyo maana tunawapa mikopo isiyo na riba ili kuwawezesha kiuchumi. Nawasihi muwe waaminifu, mfanye kazi kwa bidii na mtumie fursa hii kuboresha maisha yenu na ya familia zenu.”
Aidha, Kaganda pia amewasisitiza Vijqna hao umuhimu wa kutunza pikipiki hizo na kuzitumia vizuri kwa manufaa ya familia na jamii.

Amewataka pia kuwa mabalozi wa mfano kwa vijana wengine na kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu.
Nao Vijana hao, wakitoa neno la shukrani wameahidi kutumia fursa hiyo vyema wakidai itawasaidia kuinua maisha yao, familia na kuwa mfano mzuri kwa wasafirishaji wengine Wilayani Babati.