Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

DC Chato na waumini walaani kuvunjiwa kanisa

Baada ya tukio la watu wasiofahamika kuvamia na kuvunja ukuta wa Kanisa Katoliki la mt. Bernadetha wa lurdi Parokia ya Nyakato Buzirayombo Jimbo Katoliki la Rulenge – Ngara wilaya ya Chato Mkoani Geita, waumini wa kanisa hilo wamelazimika kuabudia nje kwa siku 30 kutokana na kufuru iliyofanyika ndani ya kanisa hilo. Jambo Fm imefika katika kijiji cha Buzirayombo mahali kanisa hilo lilipo na kukutana na waamini wa kanisa hilo wakieleza kuwa tukio hilo limetia najisi na kuathiri kwa kiasi kikubwa utakatifu wa kanisa hilo baada ya wavamizi hao kuvunja na kuingia ndani na kuharibu kwa kunywa na kutupa nje ya kanisa Ekaristi Takatifu

kutokana na tukio la kuvamiwa na kuvunjwa ukuta wa Kanisa Katoliki la mt. Bernadetha wa lurdi Parokia ya Nyakato Buzirayombo Jimbo Katoliki la Rulenge – Ngara wilaya ya Chato Mkoani Geita,Mkuu wa wilaya ya Chato Deusdetith Katwale amesema mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi akituhumiwa kuhusika na tukio hilo kwa na kulaani kitendo hicho huku akiwataka wananchi kuacha kufanya vitendo kama hivyo na badala yake waheshimu nyumba za ibada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *