Dawa feki kudhibitiwa vikali

Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Stanslaus Nyongo ameitaka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kuongeza nguvu ya kudhibiti bidhaa feki za dawa zinazoingia nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Nyongo ameyasema hayo leo Agosti 17, 2023 baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Bw. Adam Fimbo katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.

Aidha, Nyongo ameitaka Mamlaka hiyo kuangalia ufanisi wa dawa zilizopo kwa maana kuna baadhi ya dawa hazina ubora mzuri unaotakiwa kulingana na dawa husika hasa kwenye dawa wa ‘Antibiotic’.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo amesema, Usajili wa waganga wa tiba asili nchini ulianza Mwaka 2010 ambapo hadi Julai Mwaka 2023, idadi ya wataalam wa Tiba Asili/Mbadala waliosajiliwa ilifikia 47,467 na vituo vya kutolea huduma 1,640 vilikuwa vimesajiliwa.

Endelea kutufuatilia zaidi kupitia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *