Davido na Lebo Mpya,Kusaka Vipaji Vipya

Staa wa muziki, kutoka Nigeria, Davido anakamilisha wikiend yake kwa kuingia makubaliana na kampuni ya United Masters ili kuanzisha lebo mpya ya Nine+ Records.


Akitia saini mkataba huo Jumatano ya wiki hii, Davido aliweka wazi kuwa kupitia lebo hiyo hawatajihusisha na Afrobeats pekee bali watajitosa katika nyanja za muziki wa ladha tofauti tofauti ikiwemo hip-hop, R&B, Latin, country na zaidi ya yote watasaka vipaji vipya.


Staa huyo mpaka sasa anamiliki lebo ya DMW baada ya kuachana na lebo ya HKN.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *