Staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido ameweka wazi matamanio yake ya kuazisha tamasha lake litalaojumuisha wasanii wa Afrika.
Katika mahojiano aliyofanya na Apple Music, Davido amesema kuwa anatamani kuja kufanya tamasha la Are We African Yet?(A.W.A.Y) ambalo litadumisha utamaduni wa Kiafrika katika sehemu mbalimbali za dunia.