Davido atangaza ujio wa EP na Kizz daniel

Staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido ameweka wazi ujio wa EP ya pamoja kati yake na Kizz Daniel.

Hitmaker huyo wa ‘Unavailable’ ametoa taarifa hiyo kwenye mtandao wake wa kijamii  wa X kwa kuebainisha kuwa baada ya albamu yake ijayo anahisi itakuwa vizuri ikitoka EP akiwa na Kizz Daniel.

Hivi karibuni Staa wa muziki Davido alikuwa miongoni mwa mastaa wachache kutoka Afrika ambao walikuwa wakiwania tuzo za Grammy, na kwa bahati mbaya hakupata tuzo hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *