Baada ya hivi karibuni kuonekana pamoja kwenye klabu moja ya usiku, Staa wa muziki Davido na Wizkid, hatimaye ushikaji wa wawili hao umeimarika na hapo jana Davido ametangaza ujio wa EP ya Wizkid ifikapo Ijumaa.
Davido ametangaza taarifa hiyo katika ukurasa wake wa X, utakumbuka 2019 Wizkid aliacha EP yake ya ‘Soundman EP’ na hivyo ujio huo unasubiriwa kwa shauku kwani kuna dhaniwa kuna kolabo ya wawili hao.