Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Davido ageuka mbogo, adai alitoa taarifa

Staa wa muziki Davido ameomba msamaha kwa mashabiki wake wa jimbo la Delta baada ya kushindwa kutokea kutumbuiza kwenye hafla ya Warri Again iliyoandaliwa na Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Nigeria Amaju Pinnick, Oktoba 6, 2023.

Davido ambaye alilipwa dola 98,000 na waandaji ambao pia walitoa dola 18,000 kwa ndege ya kibinafsi ili kumsafirisha msanii huyo hadi Jimbo la Delta ametumia ukurasa wa X na Twitter,  kuomba radhi na pia kueleza kuwa awali aliwataarifu waandaaji wa Warri Again kuhusu kushindwa kwake kufanya shoo hiyo kutokana na muingiliano wa tarehe na tamasha lake huko New Zealand lakini waandaaji bado waliendelea kutangaza show hiyo. kwa kutumia jina lake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *