Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, Davido kwa kushirikiana na taasisi yake ya David Adeleke Foundation (DAF) wameahidi kutoa jumla ya Naira Milioni 300 ambazo ni sawa na Tsh/= 506,705,198.13 kwaajili ya kusaidia vituo vya Watoto yatima vilivyopo nchini Nigeria.

Davido ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa X na Instagram kwa kuandika “Mimi na taasisi yangu tunaahidi jumla ya Naira milioni 300 kwa vituo vya watoto yatima kote Nigeria … kama mchango wangu wa kila mwaka kwa Taifa ❤️ …

Davido ni miongoni mwa wasanii ambao mwezi huu wa Valentine ameonyesha upendo kwa kulibeba jambo la mtu mwingine kama lakwake na hii ndio maana halisi ya ‘Mimi ni Wewe’.


