Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa mlinzi, David Alaba amepata jeraha baya la goti la (ACL) ambalo huenda likamuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha msimu mzima.
Alaba alipata maumivu makali yaliyomfanya ashindwe kuendelea na mchezo katika ushindi wa 4-1 wa Real Madrid dhidi ya Villarreal kwenye mchezo wa Ligi Kuu Uhispania.
Baada ya vipimo Alaba amegundulika kuwa na jeraha hilo kwenye goti lake la mguu wa kushoto huku akitarajiwa kufanyiwa upasuaji siku zijazo.
Shughuli ya Alaba kwa msimu huu wa 2023/24 ni kama imeisha kufuatia jeraha hilo