
Mchambuzi wa mpira wa miguu nchini Tanzania Shaffih Dauda nae amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi [CCM] kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Dauda amechukua fomu hiyo leo Jumatatu Juni 30, 2025 katika ofisi za CCM Tawi la Uwanja wa Taifa, Kata ya Miburani, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Dauda ni Mkurugenzi wa Shadaka Sports lakini pia ni Mkuu wa Mahusiano ya Kimkakati wa Clouds Media Group huku ambaye amehudumu kama mchambuzi wa masuala ya michezo kwa muda mrefu.
