Daraja linalounganisha wilaya ya Geita na Nyang’hwale Mkoa wa Geita limesombwa na Maji na kupelekea wakazi wa kijiji cha Gamashi kata ya Bulela wilaya ya Geita na Wakazi wa Kijiji cha Kabhoha kata ya Kabhoha wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita kukosa mawasiliano.
Wakizungumza na Jambo Fm wananchi hao wamesema ni zaidi ya Mwezi mmoja huduma za kijamii zimekosekana kati ya wilaya hizo mbili na kuwalazimu kuzunguka Mkoa jirani wa Mwanza kufika Geita na kuiomba serikali kuwajengea daraja la Muda ili kurudisha mawasiliano kati ya wilaya hizo mbili.
Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini Na Vijijini TARURA Mkoa wa Geita Mhandisi Chacha Moseti amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema kuwaTARURA Mkoa wa Geita tayari imeomba fedha kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ya barabara ikiwemo daraja hilo na wakati wowote kuanzia sasa litaanza kurekebishwa ili kurudisha mawasiliano kati ya wilaya hizo mbili.