Mahakama ya Catalonia iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Hispania, imemuhukumu kwenda jela miaka minne na na miezi sita mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Brazil na FC Barcelona Dani Alves (40) baada ya kukutwa na hatia ya kosa la shambulio la ngono kwa Mwanamke mmoja mdogo katika Night Club.
Alves alikamatwa mara ya kwanza kwa tuhuma hizo January 2023 na amekuwa rumande toka kipindi hicho hadi ilipotolewa hukumu dhidi yake. Alves amekana makosa hayo na anaweza kukata rufaa.