Kumbusho Savani ambaye ni Daktari katika Kituo cha Afya cha Mkimbizi kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Mkoa wa Iringa amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Iringa kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 15.
Inaelezwa kuwa Mwezi Disemba 2023 binti huyo ambaye jina limehifadhiwa alikwenda katika kituo cha Afya cha Mkimbizi anapofanyia kazi Dkt. Kumbusho akiwa na dada wa kazi (House Girl) aliyekuwa akiumwa, baada ya matibabu akaomba namba ya simu ya dada huyo wa kazi kwa lengo la kuwasiliana na binti huyo.
Kwa Mujibu ya maelezo yaliyotolewa mahakani hapo Dkt. Kumbusho aliwasiliana na binti huyo kupitia namba ya dada wa kazi na wakakutana kwa mara ya kwanza na mara ya pili ndipo alimfanyia kitendo cha ukatili hapo hapo katika kituo cha Afya na alipomaliza alimpa binti huyu Shilingi Elfu 10 ili asiseme kwa mtu.