Dakika Tatu za Heshima Kwa Rais Samia Nchini korea Kusini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Causa) kwenye Sekta ya Anga na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) Hee Young Hurr nchini Korea ya Kusini hii leo Juni 3, 2024.

Zoezi hilo limefanyika ndani ya Dakika tatu na sekunde kadhaa kabla ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupata nafasi ya kutoa hotuba yake mbele ya halaiki iliyojitokeza kushuhudia hafla hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya kutunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Causa) kwenye Sekta ya Anga na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga Jijini Seoul Korea ya Kusini (Korean Aerospace University) Hee Young Hurr wa kwanza kulia, wa kwanza kushoto ni Amidi wa Shule Kuu Soo Chang Hwang.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *