Dada wa msanii wa muziki, Diamond Platnumz , Esmaplatnumz amefunga ndoa leo jioni na Meneja wa msanii wa muziki Mavokali Jembe One.
Ndoa hiyo imefungwa katika Msikiti wa Masjid Akram Uliopo Mbezi Beach, jijini Dar Es Salaam.
Hii ni ndoa ya tatu kwa Esma ambapo ya kwanza alifunga na mwanamitandao Petit Mani mnamo Septemba 20, 2014 na Julai 2020 alifunga ndoa na mfanyabiashara Yahya Msizwa, baada ya ile na Petit kuvunjika na kupata mtoto mmoja wa kike.