Msanii wa muziki kutoka lebo ya Wasafi D Voice amekutana na Katibu Mtendaji BASATA Dkt Kedmon Mapana leo kwa lengo la majadiliano yenye kujenga tasnia ya Muziki.
Majadiliano haya yamefanyika leo 29 Januari 2024 katika ofisi za Katibu Mtendaji BASATA zilizopo Maeneo ya Kivukoni jijini Dar es salaam.
Aidha katika majadiliano hayo Katibu Mtendaji alimpitisha katika kitabu cha Mwongozo wa Maadili katika kazi za Sanaa