D Voice aikaribia rekodi ya Zuchu

Mwaka 2019 msanii wa muziki Zuchu alitambulishwa na lebo ya WCB na ndani ya siku tano aliweza kufikisha wafuasi/subscribe laki moja.


Na sasa Zuchu anawafuasi zaidi ya Milioni moja na kuwa Msanii wa kwanza katika Jangwa la Sahara barani Afrika kuwa na subscribers wengi katika mtandao wa YouTube.

Sasa kijana mwingine ambaye ametambulishwa Novemba 16, mwaka huu D Voice anataka kuikaribia rekodi ya Zuchu huko Youtube. Msanii huyo mpya amefikisha subscribe laki moja kwa sasa ikiwa ni siku tisa tu tangu atambulishwe kwenye lebo hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *