HII NDIO NDOTO KUBWA ANAYOOTA CRISTIANO RONALDO KWA SASA….

Staa wa Soka Duniani Raia wa Ureno, Cristiano Ronaldo (39) ameweka wazi mipango yake ya kuwa mmiliki wa Klabu kubwa duniani kama Manchester United na zingine nyingi mara baada ya kustaafu kucheza soka la kulipwa.

CR7 (Ronaldo) ameyasema hayo akiwa kwenye hafla ya utoaji wa GLOBE SOCCER AWARDS uliofanyika siku ya Disemba 27 huko Dubai katika Falme za Kiarabu. 

Globe Soccer Awards ni tuzo zinazotolewa katika kutambua mafanikio ya watu mbalimbali wa soka. Tuzo hizo huandaliwa na Globe Soccer na kushirikisha washiriki kutoka Mashirikisho ya Kimataifa ya soka kama UEFA, UAE Pro League, ECA, na EFAA.

CR7 Kwenye mahojiano yake alisema “Mimi bado ni mdogo sana, nina mipango na ndoto nyingi sana mbeleni, lakini zingatia maneno yangu, nitakuwa mmiliki wa klabu kubwa kwa hakika”.

Kuhusu mwenendo mbovu wa timu yake ya zamani ya manchester United, Ronaldo alisema kuwa kama angekuwa mmiliki wa klabu hiyo, angeweka mambo wazi ya muhimu na kurekebisha kile anachofikiri ni tatizo ndani ya timu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *