Kamishana wa kamisheni ya Polisi Jamii CP Alex Mkama, amewataka Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali kuendelea kuzingatia maadili na kudumisha nidhamu wanapotekeleza majukumu yao.
CP Mkama ametoa maagizo hayo leo Jumamosi Agosti 22, 2026, wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya utumishi wa umoja wa askari wa Jeshi la Polisi waliohitimu depo mwaka 2011/2012 (GH Tanzania).

Amesema lengo la gizo hilo linalenga kujenga uhusiano mzuri na jamii akisisitiza kutofanya kazi kwa mazoea kutokana na mabadiliko ya kasi ya uhalifu.
Aidha, CP Mkama pia amesema Wananchi wamekuwa wakilalamikia maadili ya baadhi ya maafisa wakaguzi na askari, hivyo ni vyema kufanya kazi kwa kuzingatia weledi.


