
Klabu ya Coastal Union ya Tanga imethibitisha kuachana na aliyekua Kipa wao Raia wa Kongo Ley Ngumbi Matamp ambaye alikuwa golikipa bora wa msimu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara kwa msimu uliopita kbaada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo Disemba 10, 2024 kupitia ukurasa wao wa Instagram wameandika ‘Tumefikia makubaliano baina ya klabu yetu na golikipa wetu Ley Ngumbi Matamp ya kumaliza huduma za pande zote mbili’ – Coastal Union.

‘Uzoefu wako umechangia kwa asilimia kubwa mafanikio yetu ya msimu uliopita, Shukrani za kipekee kwa kocha wetu wa magolikipa Mansour Ally ambae alitumia nguvu na maarifa makubwa ya kurudisha uwezo na kiwango chako ukawa msaada mkubwa eneo la kulinda lango letu’ – Coastal Union
Tunakutakia kheri nyingi,na mafanikio zaidi katika maisha yako.
We will miss you, best Goalkeeper.

Matamp kabla ya kujiunga na Coastal Union msimu uliopita 2023/2024 alikua mchezaji huru akitokea FC Lupopo ya Congo, na msimu huo wa 2023/2024 Matamp aliibuka kuwa kipa bora wa msimu.


