Rapa Chrisean Rock amevunja ukimya kwa kuweka wazi kum-miss mzazi mwezake Blueface na kuamua kuchora tatto ya sura ya mweza wake katika usoni mwake.
Baby mama huyo wa Blueface ameonyesha tattoo yake mpya kwenye ukurasa wake wa Instagram. Na kuandika “#freeblueface.
Mrembo huyo pia aliwahi Kuchora Tattoo ya Blueface shingoni kwake na kuifuta kutokana na migogoro iliyokuwa ikiendelea kwenye mahusiano yao ila wiki iliyopita Chrisean alibainisha kuwa amerudi kwenye nyumba ya Blue, jambo lililowashtua mashabiki kwa kile kilichotokea mwezi Desemba 2023.