Chris Brown amvuta Arya Starr kwenye ziara yake

Staa wa muziki kutoka Nchini Marekani Chris Brown , amapa shavu mwanadada Arya Starr kutoka Nigeria kuwa miongoni mwa wageni maalumu katika ziara yake ya ‘11:11’, ambayo inatarajiwa kuanza Juni 5, 2024.

Mbali na mrembo huyo pia CB amempa shavu Muni Long kuwa mgeni rasmi.

Utakumbuka mwaka 2023 yanye ziara ya UTI, CB alimpatia nafasi mwanadada Tyla, kutoka Afrika Kusini, kutumbuiza kwenye Tour yake hiyo na hii ni kabla ya kupata umaarufu kupitia ngoma ya ‘Water’ ambayo  imempelkea mwaka huu kuwa mshindi wa tuzo kubwa za  GRAMMYs kama Best African Music Performance kupitia wimbo wake huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *