
NA EUNICE KANUMBA –SHINYANGA
UTAWALA wa jadi wa kabila la Wasukuma wa himaya ya Busiya uliopo wilayani kishapu mkoani Shinyanga hatimae umepata kiongozi mpya ambaye ni Chifu Makwaia wa tatu na tayari ameshasimikwa rasmi kwenye Ikulu ya Busiya iliyopo kata ya ukenyenge na anakuwa chifu wa 24 wa tawala hiyo kwa kuanza majukumu yake rasmi.
Himaya ya Busiya imemsimika Chifu Makwaia wa tatu baada ya chifu aliyekuwepo Edward Makwaia kuomba kustaafu baada ya kuwa kuongoza himaya hiyo kwa miaka 16 toka mwaka 2009 -2025.
katika hotuba yake ya kwanza Baada ya kusimikwa chifu Makwaia wa tatu amesisitiza neno moja kwa watu wa Busiya wawe na UPENDO ili kuijenga Busiya imara zaidi .
Kwa upande wake chifu Mstaafu Edward amesema kuwa japo amepumzika lakini bado yeye ni mwana Busiya na ataendelea kushirikiana na kiongozi mpya kwa kushiriki shughuli zote za tawala hiyo na kuwaomba viongozi na wanachi kumuunga mkono chifu Makwaia wa tatu ili aweze kufanya vizuri kuiendeleza Busiya .
Tukio la kumsimika kwa chifu huyo mpya limehudhuriwa na Balozi wa ufaransa nchini Tanzania, machifu mbalimbali, viongozi wa dini pamoja na serikali.