CHIEF MGONTO ATEMA CHECHE IKUNGI, WANA CCM WAPEWA NENO

Na Saulo Stephen – Singida.

Kampeni za ubunge katika Jimbo la Ikungi Mashariki, zimezinduliwa rasmi ambapo mgombea wa kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Thomas Mgonto maarufu kama Chief Mgonto, amenadi sera kwa Wananchi na kuomba ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo.

Uzinduzi huo, umefanyika katika viwanja vya Makiungu Wilayani Ikungi na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali, huku Mgeni Rasmi akiwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata.

Katika kampeni hizo, Mgonto, Dkt Mwigulu pamoja na makada wengine wa CCM wamenadi sera za chama hicho kwa wananchi kwa kuomba kuchaguliwa katika nafasi za Udiwani, Mbunge pamoja na kuomba wananchi na wanaikungi kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi wa Octoba 29, 2025.

Aidha, Chief Mgonto amewaahidi Wananchi wa Ikungi Mashariki kuwa atakuwa mtetezi wa maendeleo yao, kwa kuendeleza miradi iliyoanzishwa chini ya Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *