Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Chanjo ya UKIMWI yasitishwa, yaonesha haifanyi kazi

This image has an empty alt attribute; its file name is UKIMWII.png

Majaribio ya chanjo ya UKIMWI yaliyoanza katika Nchi za Tanzania, Uganda na Afrika Kusini yamesitishwa kutokana na takwimu za waliochanjwa kuonesha Chanjo waliyopata haina ufanisi katika kuzuia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI

Majaribio Hayo ambayo yalikuwa sehemu ya mpango wa PrEPVacc, ulianza Desemba 2020 ambapo ulishuhudia watu wazima 1,512 wenye Afya njema wenye umri wa miaka 18-40 kuandikishwa kupata chanjo ya kuzuia maambukizi ya VVU.

Mbali na PrEPVacc, majaribio mengine yalihusisha aina mpya ya “Oral Pre-Exposure Prophylaxis (PrEP), dawa ambayo inapunguza hatari ya kupata VVU, ili kuona kama ilikuwa na ufanisi, ambapo mradi huo bado unaendelea ukiwahusisha Watu walio hatarini zaidi wakiwemo Wanaojihusisha na Biashara ya Ngono.

Takwimu za UNAIDS zinaonesha hadi kufikia Mwaka 2022 Watu Milioni 39 walikuwa wanaishi na Maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI, Watu Milioni 37.5 wana kati ya miaka 15 na kuendelea, Watoto chini ya miaka 14 ni Milioni 1.5 na 53% ni Wanawake na Wasichana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *