Wachezaji watano wa Simba Sc akiwemo Henock Inonga, Cloutos Chama, na Shomary Kapombe wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yao baada ya kufungwa na Yanga SC mabao 5-1 siku ya jumapili
Wachezaji hao wanatuhumiwa kuihujumu timu kitendo kilichopelekea kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao
Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao cha bodi ya wakurugenzi ya Simba kilichofanyika jana jijini Dar Es Salaam
Chanzo cha uhakika kutoka Simba SC Kimesema uongozi umeshapata ushahidi wa awali kuhusu tuhuma dhidi ya wachezaji hao na sasa imeanza uchunguzi wa kina ili kujiridhisha.
Wachezaji hao watakua nje ya kambi ya timu mpaka hapo maamuzi mengine yatakapofanyika
Chanzo hicho kimesema huwenda leo klabu ya Simba ikatoa taarifa ya wazi kwa Umma juu ya maamuzi waliyofikia kuhusu wachezaji hao au wasitoe ila wahusika wamepewa taarifa.
Maamuzi mengine yaliyofikiwa na bodi ni kufutwa kazi kwa kocha mkuu Robertinho, msaidizi wake pamoja na kocha wa viungo.