CHALAMILA, TRA WAJADILI BIASHARA SAA 24 DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 18, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bwana Yusufu Mwenda katika ofisi ya mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.

RC Chalamila akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt. Toba Nguvila, amefanya mazungumzo na Kamishna huyo pamoja wataalamu wenginge waandamizi wa Mamlaka hiyo ya Mapato.

Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine RC Chalamila amezunguzia mkakati wa Mkoa kufanya biashara saa 24 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa yaliyoainishwa, ambapo kwa upande wa TRA ni fursa adhimu itakayopelekea Mamlaka hiyo kukusanya mapato zaidi ukilinganisha na sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *