Kipa wa Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Yakoub Suleiman amezawadia gari aina ya Totota Crown na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila baada ya kuiwezesha timu hiyo kufika hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwezi jana.
Zawadi hiyo imekabidhiwa hii leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondonii Jijini Dar es Salaam ambapo pia Chalamila amewazawadia wachezaji wote wa Taifa Stars walioshiriki Fainali za CHAN Viwanja na Shilingi Milioni 20.


Stars ilitinga Robo Fainali ya CHAN baada ya kuongoza Kundi B ikishinda mechi tatu na kutoa sare moja, kabla ya kutolewa na Morocco kwa bao 1-0 wakiwa nyumbani.



