CHADEMA WAHOJI ALIPO MWENYEKITI WAO TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelitaka Jeshi la Magereza, Mamlaka husika na vyombo vya dola kutoa taarifa za haraka kwa umma kuhusu mahali alipopelekwa Mwenyekiti wao Tundu Lissu kwani wana taarifa kuwa hayupo Gerezani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo Aprili 18, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia imeeleza kuwa leo ljumaa, Aprili 18, 2025, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Wakili Ali Ibrahim Juma, Mawakili, Familia na Wanachama kwa nyakati tofauti, walifika Gereza la Keko ambapoLissu anashikiliwa lakini hawakufanikiwa kumuona.

“Juhudi zao za kumuona Lissu hazikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa hayupo katika gereza hilo, cha kusikitisha, hawakupewa maelezo yoyote rasmi juu ya alipopelekwa,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *