Mahakama ya Rufani imebatilisha amri ya Mahakama Kuu iliyokuwa imekizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kushiriki katika shughuli za kisiasa.
CHADEMA, wanarudishiwa haki ya kuendelea na shughuli zake za kisiasa umetolewa hii leo Aprili 15, 2026 na jopo la majaji watatu, ambao ni Augustine Mwarija, Issa Maige na Abraham Mwampashi.
Uamuzi huo umetokana na mchakato wa mapitio ulioanzishwa na Mahakama ya Rufani kufuatia mgogoro kuhusu madai ya kuwepo kwa mgawanyo usio sawa wa rasilimali za chama kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Kesi ya msingi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu, Dar es Salaam na aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Chadema, Said Issa Mohamed, kwa kushirikiana na wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.
Waliofunguliwa kesi hiyo ni Bodi ya Wadhamini iliyosajiliwa ya chama pamoja na Katibu Mkuu wake.
Waombaji walidai kuwa kulikuwa na ukosefu wa usawa katika mgawanyo wa mali na rasilimali za kifedha za chama kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa pamoja na katiba ya chama hicho.
Qidha, waliwasilisha maombi ya muda (amri ya zuio la muda) wakitaka kuwazuia walalamikiwa kushiriki shughuli za kisiasa au kutumia mali za chama hadi kesi ya msingi itakapoamuliwa.


