Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mhe. Tundu Antiphas Lissu anatarajiwa kuripoti Makao Makuu ya Chama Mikocheni, Dar Es salaam Januari 29, 2025 ili kuanza rasmi majukumu yake mapya.
Taarifa iliyotolewa na Msaidizi wa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya nje, Apolinary Boniface Margwe imeeleza kiwa Lissu ataambatana na Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. John Heche na Naibu Katibu Mkuu Bara Mhe. Amani Golugwa.
“Mhe. Lissu na ujumbe wake utapokelewa na Katibu Mkuu wa Chama Mhe. John Mnyika pamoja na watendaji wa Makao Makuu. Itakumbukwa Mwenyekiti alichaguliwa katika Mkutano Mkuu wa Chama Taifa uliofanyikatarehe 21 Januari 2025 Mlimani City Dar Es salaam,” ilieleza taarifa hiyo.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250128-WA0050-816x1024.jpg)
Aidha, imearifiwa kuwa CHADEMA inawakaribisha Viongozi Wakuu wa Chama kutoka Zanzibar, Viongozi Wakuu wa Mabaraza ya Chama, Viongozi wa Kanda ya Pwani na viongozi kutoka maeneo mengine Makao Makuu ya Chama kumsindikiza Lissu akiripoti rasmi Makao Makuu ya Chama.
“Vilevile Chama kinawakaribisha Waaandishi wa Habari Makao Makuu ya Chama siku hiyo na Mwenyekiti atazungumza na vyombo vya habari ikiwa ni siku yake ya kwanza kazini,” alieleza.