Mkongwe wa muziki wa Pop Dunia, Celine Dion, ambaye anaugua ugonjwa wa neva, ameongea kwa mara ya kwanza katika mahojiano yake na toleo la Jarida la Vouge France, linalotarajiwa kutoka mwezi Mei, mwaka huu ambapo mahojiano hayo yamejikita katika ugonjwa huo.
Nyota huyo amedai kuwa anaamini kuwa amepona ugaonjwa huo, lakini hali yake inahitaji msaada mwingi, ili kuweza kuwa sawa kwani ugonjwa huo hauna dawa mpaka sasa.
“Siku tano kwa wiki mimi huwa napata matibabu ya riadha, ya mwili na ya sauti. Sijashinda ugonjwa huo, kwani bado uko ndani yangu na itakuwa hivyo kila wakati. Natumaini kwamba nitapata miuujiza, kwa njia ya kuuponya kwa utafiti wa kisayansi, lakini kwa sasa, ni lazima nijifunze kuishi nao.”Amesema Celine
Celine aliweka wazi kwa mara ya kwanza kuwa mnamo Desemba 2022 ndipo alipogundulika kuwa anaugua ugonjwa huo.