CCM SHINYANGA YATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WALIOSHINDA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KISHAPU.

NA EUNICE KANUMBA -KISHAPU

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Ndg, Mabala  Mlolwa Disemba 13 2024 amefanya ziara wilaya ya Kishapu na  kuzungumza na Wenyeviti wa Serikali za vijiji 117 na wenyeviti wa vitongoji 605 waliochaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika November 27 2024 kwa lengo la kuwapongeza kwa kuchaguliwa lakini pia kuwapa mafunzo ya utendaji kazi.

Mabala amewataka viongozi hao wachape kazi kwa weledi katika kuwatumikia wananchi bila kuwabagua kwa Udini, Ukabila, Rangi na wala vyama vyao huku akianisha kuwa wote ni Watanzania na kuwataka kutatua kero za wananchi na kukemea rushwa ili kutowakandamiza wanyonge huku akiweka wazi kuwa wataokwenda kinyume na taratibu za chama hicho watachukuliwa hatua.

Aidha, Mwenyekiti Mabala amewasisitiza Wenyeviti wa vijiji  na Vitongoji  kufanya mikutano kwenye maeneo yao nakuwashukuru wananchi pamoja  na kusikiliza changamoto za wananchi na kuzishugulikia, changamoto zilizo juu yao wazipeleka panapo husika ili ziweze kufanyiwa kazi.

Ndg, Mabala amewakumbusha pia kuendelea kuisemea miradi yote iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sababu kila Kijiji na kitongoji kimefikiwa na mradi wa kimaendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *