Na Frank Aman, Geita.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Steven Wasira amesema Chama hicho kimejiandaa kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu katika Mazingira Huru na ya Haki.

Akizungumza Siku ya Jana na Wakazi wa Mji Mdogo wa Katoro Mkoani Geita, Wasira amesema kuwa Ushindi huo wa CCM utatokana na kukamilika kwa Miradi mingi ya Maendeleo kama Ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), Reli ya Kisasa ya SGR, Vituo vya Afya ikiwemo Hospitali, Uboreshwaji wa Sekta ya Elimu pamoja na ujenzi wa Daraja la John Pombe Magufuli lililoko katika eneo la Busisi linaunganisha Mkoa wa Mwanza na Geita utamuwezesha Rais Samia Suluhu Hassan kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi huo wa Mwezi Oktoba Mwaka huu.
Wasira amewaambia Wakazi wa eneo hilo kuwa Chama hicho hakitavumilia jaribio lolote la kutaka kuvunja Umoja wa Nchi na amani iliyopo na kuongeza kuwa Watu wanao fikiria kufanya hivyo mpango wao hautaweza kutimia.
Wasira amesema CCM itaendelea kuwaletea Wananchi Maendeleo Maendeleo yanayogusa Maisha yao bila kujali Itikadi zao huku akiwa tahadharisha Wagombea wa nafasi mbali mbali za Uongozi kwa ngazi za Udiwani, Ubunge waliochaguliwa katika nafasi hizo katika Uchaguzi Mkuu uliopita wajipime kama wamewatumikia Wananchi katika nafasi zao walizopata uchaguzi uliopita kabla ya kurudi Tena kuwania nafasi hizo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Geita Hashim Komba ambaye alizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela amesema kuwa katika Mkoa wa Geita Ilani ya CCM imetekelezwa kwa asilimia Mia Moja na Wananchi wameridhishwa na Utekelezaji wake.
Naye Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Geita, Charles Kazungu amesema kuwa hadi kufikia Mwaka huu wa 2025, Sekta ya Elimu imeendelea kuboreshwa ambapo katika eneo la Katoro na Ludena sasa zina Shule za Sekondari 12 ambazo zimekuwa na mchango Mkubwa katika Sekta hiyo Mkoani humo.
Katika Mkutano huo wa hadhara baadhi ya Wananchi na Wakazi wa eneo la Katoro, Mkoa wa Geita akiwemo Rhobi Chacha ametoa ombi lake kwa Wasira akimtaka awasaidie Wajane kwa kuwapatia Mikopo kwa kuwa Waume zao wamepoteza Maisha katika Shughuli za Uchimbaji wa Madini.