Card B athibitisha kuachana na Offset

Rapa Cardi B amethibitisha kuachana na mumewe Offset ambaye wamekuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka mitano.

Cardi B amesema yupo Single kupitia Live aliyofanya Instagram, “Nimekuwa single kwa dakika moja sasa. Lakini nimekuwa nikiogopa…siogopi, sijui tu kuuambia ulimwengu,” alisema mrembo huyo.


“Mara ya mwisho nilipoenda Live, nilitaka kuwaambia, lakini sikujua jinsi ya kuwaambia hivyo nilibadilisha mawazo yangu. Lakini imekuwa hivi kwa sasa,” aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *