CAG MSTAAFU UTOUH AWAFUNDA VIONGOZI NAMNA YA KUTHIBITI UBADHILIFU NCHINI

Shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha imeaanza kutoa mafunzo kwa viongozi wa taasisi za serikali na mashirika ya Umma nchini ikiwa mkakati wa kumaliza ubadhilifu wa fedha za Umma katika kushughulikia makosa yaliyobainika katika taarifa ya mkaguzi Mkuu wa serikali CAG.

Mkuu wa Shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Prof. Marceline Chijoriga akimkaribisha Mgeni rasmi kwa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkaguzi Mkuu wa serikali mstaafu CAG Ludovick Utouh amesema washiriki 40 kutoka taasisi za serikali, binafsi na mashirika ya Umma ya hapa nchini wapo shuleni hapo kwa siku tano kujifunza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja uongozi bora, uzalendo ikiwa ni pamoja na usimamizi bora wa taasisi na mashirika ya Umma yajiendeshe kwa faida.

Alisema kiongozi wa juu ya taasisi za serikali na mashirika ya Umma ndio wanadhamana ya kuhakikisha taasisi na shirika la Umma linafanikiwa hata kuleta faida kwenye taifa.

Aidha aliwahoji washiriki hao wa mafunzo na kutafuta majibu katika taasisi yake kutafutia majibu Nini kinasababisha taasisi za serikali na mashirika ya Umma kushindwa kujiendesha kwa mafanikio hata kusababisha Kila mwaka taifa linapata taarifa za Mkaguzi Mkuu wa serikali CAG zenye makosa ya ubadhilifu wa fedha za Umma.

Mkaguzi Mkuu wa serikali mstaafu CAG Ludovick Utoh aliwataka viongozi hao wa taasisi za serikali na mashirika ya Umma nchini kuhitimisha Mafunzo hayo kwa kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kumaliza tatizo la ubadhilifu wa fedha za Umma katika kuendesha taasisi za serikali na mashirika ya Umma nchini.

Amesema Kuna umuhimu mkubwa wa serikali kupitia ofisi ya msajili wa Hazina kutengeneza timu ya Wataalamu wafanye uchambuzi yakinifu ya mashirika ya Umma na taasisi za serikali ambayo yanapata hasara na yataweza kuendelea kupata hasara na kuendelea kusababishia hasara nchi.

“Katika uchambuzi huo waangalie kiini cha hasara hizo zinatokana na nini kwasababu kwa bahati mbaya sheria zetu hapa nchini hazitofautishi sheria hii inagusa shirika la Umma la biashara au shirika la Umma la kutoa huduma.

Akizungumzia sheria ya manunuzi ya Umma amesema inatakiwa itekelezwe na mashirika ya Umma na taasisi za serikali ili kufanya kazi kwa faida.

“Kuna umuhimu mkubwa sana wa Nchi YETU kuhimarisha ofisi ya mkaguzi Mkuu wa ndani kwani Ofisi yenye umuhimu mkubwa kwaajili ya ufanisi wataasisi za Umma hapa nchini” alisema.

Alisema Kuna haja ya kutengeneza sheria ya kuhimarisha hiyo Ofisi na kuiwekea namna ya kuiangalia utendaji wake wa kazi ufanyike vipi hata taarifa yake ya mwaka ifike hadi kwenye Baraza la mawaziri na.kutafutiwa ufumbuzi.

Naye Mkurugenzi wa taasisi ya Amo foundation Amina Saidi amesema mafundisho hayo ya siku tano yatakuwa chachu ya utendaji kazi wake katika kuwahudumia jamii kwani ilikuweza kufanya kazi vizuri ni lazima apate Mafunzo hayo ya uongozi, utawala bora, uzalendo.

Na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Simbani ya wilayani Kibaha Zamda Komba amesema Mafunzo hayo yatamsaidia katika utendaji kazi wake hasa katika kusimamisa rasrimali za shule kwa uongozi wenye tija kwa taifa na kumsaidia kufanya vizuri katika jamii wanazoziongoza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *