Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limezipiga faini timu za taifa za Morocco na Senegal pamoja na kuwasimamisha wachezaji na makocha wao kwa mechi zijazo za CAF, katika matukio yaliyotokea wakati wa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 uliyofanyika 18 Januari 2026 mjini Rabat nchini Morocco.
Kamati ya Nidhamu CAF imeeleza kuwa, adhabu hiyo imetolewa kufuatia matukio ya ukiukwaji wa maadili na kanuni za nidhamu katika Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, iliyofanyika nchini Morocco.
MCHANGANUO WA ADHABU:
1- Kocha wa Senegal Pape Thiaw amefungiwa mechi tano rasmi pamoja na faini ya dola 100,000 za Kimarekani sawa na Million 240 za Kitanzania.

2- Mchezaji wa Senegal Malick Ndiaye amefungiwa mechi mbili.
3- Mchezaji Ismaila Sarr wa Senegal amefungiwa mechi mbili.
4- Shirikisho la soka la Senegal limepigwa faini ya dola 300,000 sawa na Million 760 za Kibongo, wakiwapiga Faini kutokana na vurugu za Mashabiki wao.
5- Senegal tena wamepigwa faini ya dola 300,000 za Kimarekani kutokana na vurugu za Wachezaji na benchi la Ufundi.

6- Senegal wamepigwa faini ya dola 15,000 kutokana na Wachezaji wake kupokea kadi nyingi za onyo.
7-Nyota wa Morocco Achraf Hakimi amefungiwa mechi mbili ila atatumikia moja halafu moja kwa uangalizi wa mwaka.
8- Nyota wa Morocco Ismael Saibari amefungiwa mechi tatu na faini ya dola 100,000 za Kimarekani.

9- Morocco wamepigwa faini jumla ya dola 315,000 za Kimarekani kutokana na vurugu za Mashabiki, Wachezaji na matumizi ya tochi kwa Mashabiki.
Adhabu kwa Mashirikisho ni SENEGAL wanapaswa kulipa dola 615,000 za Kimarekani huku MOROCCO wanapaswa kulipa dola 315,000 za Kimarekani.
#jambo fm radio


