CAF YAUFUNGIA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA

Kutokana na eneo la kuchezea (Pitch) kuendelea kupungua ubora, Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), limeufungia kwa muda Uwanja wa Benjamin Mkapa.

CAF imeelekeza eneo hilo liboreshwe haraka kufikia viwango vinavyotakiwa ili kuepuka Uwanja huo kufungiwa kwa muda mrefu huku mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAF CC) kati ya Simba na Al Masry ya Misri ikipangwa kuchezwa kwenye uwanja huo Aprili 9, 2025.

Kufuatia hali hiyo,, Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), limetakiwa kutuma jina la uwanja mbadala, utakaotumiwa na Simba SC hadi kufikia Machi 14, 2025.

Aidha, CAF imeeleza kuwa itafanya ukaguzi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa Machi 20, 2025, ili kuona maboresho yaliyofanyika kabla ya kuuruhusu utumike.

Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo jijini Dar es salaam pia umepangwa kutumika kwa ajili ya Fanali za CHAN zinazotarajiwa kufanyika Agosti 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *