Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kilwa Kusini Ndugu Suleiman Bungara (Bwege) amejitosa kugombea Ujumbe wa Kamati Kuu wa ACT Wazalendo.
Bwege aliyekua maarufu kwa Bunge lililopita kwa misemo yake kama ‘Tunaanza upya’ na ‘Wewe ulisikia wapi’ amekabidhiwa fomu hiyo na Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Uchaguzi Ndugu Joran Bashange ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Bara.