Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Burundi Yaomba Msaada Kukabili Mafuriko

Serikali ya Burundi kwa ushirikiano na Umoja wa mataifa imetoa wito wa kupatiwa msaada wa haraka ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Gavana wa mkoa wa Bujumbura vijijini Desire Nsengiyumva amesema watu 7 wamepoteza maisha baada ya kuliwa na kiboko na wanyama wengine, na kwamba zoni za Rukaramo na Gatumba kwenye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ndio ziloathiriwa zaidi na kwamba inafanyika sensa ili waweze kuhamishiwa katika maeneo yaliyo salama.

Katika Tamko la pamoja la waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Martin Niteretse na msimamizi wa matawi ya Umoja wa mataifa nchini humo bi Violette Kakyoma wametoa wito wa msaada wa haraka ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Watu zaidi ya laki 3 wanahitaji misaada huku wakisema makadirio ya hali ya hewa yanaonesha kuwa mvua bado zitaendelea kunyesha na Burundi ni miongoni mwa nchi 20 duniani zinazo zinazoshuhudia athari ya mabadiliko ya tabia nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *