BURUNDI INAUTAMANI MZOZO WA DRC? YAIONYA RWANDA

Rais wa Burundi Evariste Ndashimiye ameonya kuwa yeyote atakayeishambulia nchi yake naye atashambuliwa, huku Miji ya Ihusi na Kalehe, iliyoko karibu kiliomita 60 kutoka Bukavu immkiwa imetekwa.

Kauli ya Ndashimiye inakuja wakati ambao Wapiganaji wa M23 na Askari wa Rwanda wakiendelea kusonga mbele katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

Tayari Serikali ya Kinshasa imeitisha mkutano wa dharura wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kutathmini hali hiyo na huku ikitoa wito wa vikwazo kwa Rwanda.

Hata hivyo, Kauli ya Ndashimiye inakuja huku ikidaiwa kuwa Madaktari wa Nchini mwake wanavuka mpaka kwenda kuhudumu mataifa ya ugenini, kutokana na sekta ya afya ya Burundi kukabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo malipo duni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *