Burna Boy, Rema na Asake waitwa Brit

Waandaji wa tuzo kubwa za muziki nchini Uingerzea, Brit wametoa oradha ya wasanii wanaowania tuzo hizo kwa mwaka 2024, huku Afika ikiwakilishwa na Burna Boy, Asake na Rema.

Burna Boy na Asake wameteuliwa kuwania  kipengele cha Msanii Bora wa Kimataifa , ambapo wanachuwana na magwiji wa Marekani Taylor Swift, Miley Cyrus, Sza, Olivia Rodrigo, na Lana Del Rey.

Rema ameteuliwa kipengele cha Wimbo Bora wa Kimataifa kwa wimbo wake wa ‘Calm Down’.

Wengine waliotjwa ni Libianca na mkali wa Afrika Kusini anayekuja kwa kasi Tyla kwa rekodi yake kali ya ‘Water’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *