Ngoma ya ‘City ya Burna Boy imetajwa kuwania tuzo za Grammy kipengele cha ‘Best African Music Performance’, Pia ‘Alone’ itawania kipengele cha ‘Best Global Music Performance’, na albamu yake ya ‘I Told Them’ ipo kipengele cha ‘Best Global Album’, vile vile kupitia rap aliyofanya na 21 Savage ‘Sittin’ imetajwa kwenye ‘ Best Melodic Rap Performance’.

Staa huyu anaingia mara nne kwenye tuzo hizi kubwa za Grammy na Burnaboy ana kuwa msanii wa kwanza Barani Afrika kuwa kwenye mfululizo wa tuzo hizo tangu 2019 hadi 2023.