Rapa kutoka Marekani Busta Rhymes, ameweka wazi kufanya kazi na Burna Boy ni moja ya mafanikio makubwa sana kwa upande wake wa muziki.

Busta ametoa kauli hiyo katika mahojiano aliyofanya kwenye Capital Xtra Podcast.
“Kufanya kazi na Burna Boy ilikuwa mojawapo ya matukio mema sana niliyopitia kwenye maisha yang. Kwa sababu ana kasi, ana ufanisi na nimkweli sana, anajua anachokitaka na anachofanya, hana muda wa kupotezi,” amesema Busta.
Burna ni miongoni mwa wasanii waliopata nafasi katika wimbo ‘Roboshotta’ kutoka albamu ya Busta Rhymes,iitwayo ‘Blockbusta’.